
Serikali
imedhamiria kuviimarisha na kuvijengea uwezo vituo vya vijana ili viweze
kutoa mafunzo kwa vijana wengi zaidi hali ambayo itasaidia vijana
kujiajili na kujipatia kipato pamoja na kuliendeleza Taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Bw. Sethi Kamuhanda alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya
Vijana Ilonga kilichopo wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
“Lengo
kubwa la Serikali kuanzisha vituo vya vijana ni kutaka vitoe mafunzo ya
ujasiriamali kwa vijana ili wawe na uwezo wa kujiajiri na kujitegemea.”
Amesema Bw. Kamuhanda.
Aidha,
Bw. Kamuhanda amesema kuwa Serikali imedhamiria kuimarisha Mfuko wa
Vijana ili vikundi vingi zaidi vya vijana viweze kukopeshwa kwa ajili ya
kufanikisha shughuli za kiuchumi na kutokomeza umaskini.
Amesema
kuwa kwa sasa Mfuko huo unatoa mikopo kwa vikundi vya vijana kupitia
saccos zilizoainishwa na halmashauri ambazo vikundi hivyo vinatokea
lakini bado hautoshelezi mahitaji kwani fedha inayotengwa kwenye mfuko
huo ni ndogo ukilinganisha na mahitaji yaliyopo.
Naye
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana Ilonga, Bw. Ombeni Andrew
amesema kuwa Kituo hicho kinatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana,
utunzaji wa mazingira, masuala yanayohusu VVU/UKIMWI na mafunzo ya
Teknolojia ya habari na mawasiliano.
“Lengo
hasa la kuanzisha somo la Teknolojia ya habari na mawasiliano
(TEKNOHAMA) chuoni hapo ni kutaka vijna kupata habari mbalimbali
zinazohusu vijana hususan zile zinazohusu masuala ya UKIMWI kupitia
mtandao wa intaneti ili wawe na uwezo wa kujikinga na ugonjwa huo”.
Amesema Bw. Andrew.
Ameeleza
kuwa vikundi mbalimbali vya vijana vimekuwa vikifika kituoni hapo kwa
nyakati tofauti kulingana na mahitaji ya wakati huo na wamekuwa
wakiwapatia mafunzo ya ujasiriamali na wakati mwingine uzarishaji mali
kama vile kutengeneza mkaa wa nyasi ambao husaidia kutunza mazingira.
Akielezea
namna wanavyowahudumia vijana wanaofika chuoni hapo kwa ajili ya
kujifunza, Bw. Andrew amesema kuwa Kituo kina mabweni yenye uwezo wa
kulaza vijana 48 na chakula kinapikwa hapo kituoni kwa ajili ya
wanafunzi.
Kaimu
Mkuu huyo wa kituo ametoa wito kwa Serikali kuanzisha programu za
mafunzo nyingi zaidi na kutafuta watumishi sahihi na wa kutosha kwa
ajili ya kuendesha mafunzo hayo.
Kituo cha
Maendeleo ya Vijana Ilonga ni moja kati ya vituo vitatu vya maendeleo
ya vijana ambavyo viko chini ya usimamizi wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo. Vituo vingine ni Sasanda kilichopo wilayani Mbozi
Mkoani Kilimanjaro na Kituo cha Vijana Marangu cha Mkoani Kilimanjaro.
misaada mbalimbali yaendelea kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwasaidia waliofikwa na janga la mafuriko
baadhi ya vifaa vya misaada iliyotolewa.





imetolewa na SAM SHEMSANGA kwa msaada wa mtandao
Casino Roll
ReplyDeleteCasino Roll is 해외 축구 스코어 a trusted, trusted and easy-to-use 스포츠 토토 gambling 메이플 캐릭터 슬롯 platform that's 커뮤니티 모음 safe and secure. We offer casino slots, 파라오 사이트 video poker, live dealer games, online