Wednesday 7 May 2014

SERIKALI YAPANIA KUIMARISHA VITUO VYA VIJANA


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Sethi Kamuhanda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana Ilonga, Bw. Ombeni Andrew kuhusu Kompyuta zinazotumika kufundishia mafunzo ya TEKNOHAMA kituoni hapo. Bw. Kamuhanda alitembelea Kituo hicho mwanzoni mwa wiki hii kwa ajili ya kukagua maendeleo ya kituo hicho.
 
Serikali imedhamiria kuviimarisha na kuvijengea uwezo vituo vya vijana ili viweze kutoa mafunzo kwa vijana wengi zaidi hali ambayo itasaidia vijana kujiajili na kujipatia kipato pamoja na kuliendeleza Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Sethi Kamuhanda alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya Vijana Ilonga kilichopo wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

“Lengo kubwa la Serikali kuanzisha vituo vya vijana ni kutaka vitoe mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana ili wawe na uwezo wa kujiajiri na kujitegemea.” Amesema Bw. Kamuhanda.

Aidha, Bw. Kamuhanda amesema kuwa Serikali imedhamiria kuimarisha Mfuko wa Vijana ili vikundi vingi zaidi vya vijana viweze kukopeshwa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kiuchumi na kutokomeza umaskini.

Amesema kuwa kwa sasa Mfuko huo unatoa mikopo kwa vikundi vya vijana kupitia saccos zilizoainishwa na halmashauri ambazo vikundi hivyo vinatokea lakini bado hautoshelezi mahitaji kwani fedha inayotengwa kwenye mfuko huo ni ndogo ukilinganisha na mahitaji yaliyopo.

Naye Kaimu Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana Ilonga, Bw. Ombeni Andrew amesema kuwa Kituo hicho kinatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana, utunzaji wa mazingira, masuala yanayohusu VVU/UKIMWI na mafunzo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano.

“Lengo hasa la kuanzisha somo la Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) chuoni hapo ni kutaka vijna kupata habari mbalimbali zinazohusu vijana hususan zile zinazohusu masuala ya UKIMWI kupitia mtandao wa intaneti ili wawe na uwezo wa kujikinga na ugonjwa huo”. Amesema Bw. Andrew.

Ameeleza kuwa vikundi mbalimbali vya vijana vimekuwa vikifika kituoni hapo kwa nyakati tofauti kulingana na mahitaji ya wakati huo na wamekuwa wakiwapatia mafunzo ya ujasiriamali na wakati mwingine uzarishaji mali kama vile kutengeneza mkaa wa nyasi ambao husaidia kutunza mazingira.

Akielezea namna wanavyowahudumia vijana wanaofika chuoni hapo kwa ajili ya kujifunza, Bw. Andrew amesema kuwa Kituo kina mabweni yenye uwezo wa kulaza vijana 48 na chakula kinapikwa hapo kituoni kwa ajili ya wanafunzi.

Kaimu Mkuu huyo wa kituo ametoa wito kwa Serikali kuanzisha programu za mafunzo nyingi zaidi na kutafuta watumishi sahihi na wa kutosha kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo.

Kituo cha Maendeleo ya Vijana Ilonga ni moja kati ya vituo vitatu vya maendeleo ya vijana ambavyo viko chini ya usimamizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Vituo vingine ni Sasanda kilichopo wilayani Mbozi Mkoani Kilimanjaro na Kituo cha Vijana Marangu cha Mkoani Kilimanjaro.
 

misaada mbalimbali yaendelea kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwasaidia waliofikwa na janga la mafuriko

 baadhi ya vifaa vya misaada iliyotolewa.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya misaada iliyotolea na Umoja wa Masheikh na Wanazuoni wa Nchini Tanzania wenye jumla ya thamani ya sh. Milioni 12,kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo,Sheikh Hamis Mataka (mwenye kanzu nyeusi) leo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.Wengine pichani ni wajumbe wa Umoja huo wa Masheikh.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Masheikh na Wanazuoni Nchini,Sheikh Hamis Mataka (katikati) akisoma taarifa fupi ya misaada mbali mbali iliyotolewa na umoja huo kwa ajili ya waathirika wa janga la Mafuriko lililolikumba jiji la Dar es Salaam hivi karibuni wakati walipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (wa pili kulia) leo kwa ajili ya kukabidhi msaada huo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq akitoa shukrani kwa wale woote waliofika ofisini kwake leo kwa lengo la kuwasilisha midaada mbalimbali kwa ajili wa waathirika wa Mafuriko yaliyotokea hivi karibu jijini Da
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kulia) akipokea Misaada ya vyakula kutoka kwa vijana wanaounda Muungano wa Mashirika ya Vijana nchini,Kushoto ni Kiongozi wa Muundano huo,Nyakia Ally na Katikati ni Mjumbe wa Muungano huo,Sostenes Mitt
 Kiongozi wa Muungano wa Mashirika ya Vijana nchini,Nyakia Ally (kushoto) akiongea na vyombo vya habari wakati wa kukabidhi sehemu ya misaada kwa ajili ya waathirika wa Mafuriko jijini Dar es Salaam wakati walipofika kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kulia) kukabidhi misaada yao hiy
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa ya Meneja Mauzo wa DarBrew LTD ambao ni Watengenezaji wa Kinywaji cha Chibuku,Urban Shayo wakati walipofika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kukabidhi Msaada wao kwa waathirika wa Mafuko
imetolewa na SAM SHEMSANGA kwa msaada wa mtandao

1 comment:

  1. Casino Roll
    Casino Roll is 해외 축구 스코어 a trusted, trusted and easy-to-use 스포츠 토토 gambling 메이플 캐릭터 슬롯 platform that's 커뮤니티 모음 safe and secure. We offer casino slots, 파라오 사이트 video poker, live dealer games, online

    ReplyDelete