Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Sethi
Kamuhanda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha Maendeleo
ya Vijana Ilonga, Bw. Ombeni Andrew kuhusu Kompyuta zinazotumika
kufundishia mafunzo ya TEKNOHAMA kituoni hapo. Bw. Kamuhanda alitembelea
Kituo hicho mwanzoni mwa wiki hii kwa ajili ya kukagua maendeleo ya
kituo hicho.
Serikali
imedhamiria kuviimarisha na kuvijengea uwezo vituo vya vijana ili viweze
kutoa mafunzo kwa vijana wengi zaidi hali ambayo itasaidia vijana
kujiajili na kujipatia kipato pamoja na kuliendeleza Taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Bw. Sethi Kamuhanda alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya
Vijana Ilonga kilichopo wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
“Lengo
kubwa la Serikali kuanzisha vituo vya vijana ni kutaka vitoe mafunzo ya
ujasiriamali kwa vijana ili wawe na uwezo wa kujiajiri na kujitegemea.”
Amesema Bw. Kamuhanda.
Aidha,
Bw. Kamuhanda amesema kuwa Serikali imedhamiria kuimarisha Mfuko wa
Vijana ili vikundi vingi zaidi vya vijana viweze kukopeshwa kwa ajili ya
kufanikisha shughuli za kiuchumi na kutokomeza umaskini.
Amesema
kuwa kwa sasa Mfuko huo unatoa mikopo kwa vikundi vya vijana kupitia
saccos zilizoainishwa na halmashauri ambazo vikundi hivyo vinatokea
lakini bado hautoshelezi mahitaji kwani fedha inayotengwa kwenye mfuko
huo ni ndogo ukilinganisha na mahitaji yaliyopo.
Naye
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana Ilonga, Bw. Ombeni Andrew
amesema kuwa Kituo hicho kinatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana,
utunzaji wa mazingira, masuala yanayohusu VVU/UKIMWI na mafunzo ya
Teknolojia ya habari na mawasiliano.
“Lengo
hasa la kuanzisha somo la Teknolojia ya habari na mawasiliano
(TEKNOHAMA) chuoni hapo ni kutaka vijna kupata habari mbalimbali
zinazohusu vijana hususan zile zinazohusu masuala ya UKIMWI kupitia
mtandao wa intaneti ili wawe na uwezo wa kujikinga na ugonjwa huo”.
Amesema Bw. Andrew.
Ameeleza
kuwa vikundi mbalimbali vya vijana vimekuwa vikifika kituoni hapo kwa
nyakati tofauti kulingana na mahitaji ya wakati huo na wamekuwa
wakiwapatia mafunzo ya ujasiriamali na wakati mwingine uzarishaji mali
kama vile kutengeneza mkaa wa nyasi ambao husaidia kutunza mazingira.
Akielezea
namna wanavyowahudumia vijana wanaofika chuoni hapo kwa ajili ya
kujifunza, Bw. Andrew amesema kuwa Kituo kina mabweni yenye uwezo wa
kulaza vijana 48 na chakula kinapikwa hapo kituoni kwa ajili ya
wanafunzi.
Kaimu
Mkuu huyo wa kituo ametoa wito kwa Serikali kuanzisha programu za
mafunzo nyingi zaidi na kutafuta watumishi sahihi na wa kutosha kwa
ajili ya kuendesha mafunzo hayo.
Kituo cha
Maendeleo ya Vijana Ilonga ni moja kati ya vituo vitatu vya maendeleo
ya vijana ambavyo viko chini ya usimamizi wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo. Vituo vingine ni Sasanda kilichopo wilayani Mbozi
Mkoani Kilimanjaro na Kituo cha Vijana Marangu cha Mkoani Kilimanjaro.
misaada mbalimbali yaendelea kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwasaidia waliofikwa na janga la mafuriko
baadhi ya vifaa vya misaada iliyotolewa.
Katibu Mkuu
wa Umoja wa Masheikh na Wanazuoni Nchini,Sheikh Hamis Mataka (katikati)
akisoma taarifa fupi ya misaada mbali mbali iliyotolewa na umoja huo kwa
ajili ya waathirika wa janga la Mafuriko lililolikumba jiji la Dar es
Salaam hivi karibuni wakati walipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (wa pili kulia) leo kwa ajili ya
kukabidhi msaada huo
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq akitoa shukrani kwa wale woote
waliofika ofisini kwake leo kwa lengo la kuwasilisha midaada mbalimbali
kwa ajili wa waathirika wa Mafuriko yaliyotokea hivi karibu jijini Da
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kulia) akipokea Misaada ya
vyakula kutoka kwa vijana wanaounda Muungano wa Mashirika ya Vijana
nchini,Kushoto ni Kiongozi wa Muundano huo,Nyakia Ally na Katikati ni
Mjumbe wa Muungano huo,Sostenes Mitt
Kiongozi wa
Muungano wa Mashirika ya Vijana nchini,Nyakia Ally (kushoto) akiongea na
vyombo vya habari wakati wa kukabidhi sehemu ya misaada kwa ajili ya
waathirika wa Mafuriko jijini Dar es Salaam wakati walipofika kwa Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kulia) kukabidhi misaada
yao hiy
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kushoto) akisikiliza kwa makini
taarifa ya Meneja Mauzo wa DarBrew LTD ambao ni Watengenezaji wa
Kinywaji cha Chibuku,Urban Shayo wakati walipofika ofisini kwa Mkuu wa
Mkoa kwa ajili ya kukabidhi Msaada wao kwa waathirika wa Mafuko
imetolewa na SAM SHEMSANGA kwa msaada wa mtandao
Casino Roll
ReplyDeleteCasino Roll is 해외 축구 스코어 a trusted, trusted and easy-to-use 스포츠 토토 gambling 메이플 캐릭터 슬롯 platform that's 커뮤니티 모음 safe and secure. We offer casino slots, 파라오 사이트 video poker, live dealer games, online